Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA NA MSIMU M’BOVU….MASHABIKI MAN UTD WAONYESHA UBABE…WANUNUA TIKETI ZOTE...

PAMOJA NA KUWA NA MSIMU M’BOVU….MASHABIKI MAN UTD WAONYESHA UBABE…WANUNUA TIKETI ZOTE …..


Ama kweli, mkubwa ni mkubwa. Licha ya kuwa na msimu mbovu 2021/22, Manchester United imeshauza tiketi zote za msimu ujao, 2022/23.

Old Trafford ni uwanja mkubwa zaidi Uingereza unaomilikiwa na klabu. Ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 74,000, Man United mara zote inawekaga tiketi zaidi ya 50,000 kwa ajili ya mashabiki wanaonunua tiketi za msimu mzima.

Ikiwa ni juzi tu msimu umeisha na Jana Erik Ten Hag kuanza majukumu yake rasmi kama kocha mkuu wa United, klabu hiyo imetangaza kumaliza mauzo ya tiketi kwa mashabiki wanaonunua tiketi za msimu mzima.

Hii ni nguvu ya ajabu ambayo, mashabiki wa klabu hiyo wamekua nayo wakionesha mapenzi makubwa kwa timu yao licha ya kuwa katika nyakati ngumu kwenye kupata matokeo.

2022 ni mwaka wa 9 toka The Red Devils walipotwaa taji la EPL na, hata hivyo ukame wa makombe umeendelea toka Sir Alex Ferguson alipostaafu kuiongoza klabu hiyo. 2022/23 utakua msimu wa aina gani chini ya Ten Hag?

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO....TARAJIA KUONA KIUNGO HUYU MJANJA MJANJA AKIKIPIGA MSIMBAZI...NI ZAIDI YA MIQUISSONE...