Home CAF PITSO MOSIMANE NA AL AHLY KUANDIKA HISTORIA MPYA LEO…NI WAARABU vs WAARABU...

PITSO MOSIMANE NA AL AHLY KUANDIKA HISTORIA MPYA LEO…NI WAARABU vs WAARABU LIGI YA MABINGWA AFRIKA…


Kocha wa klabu ya Al Ahly, Pitso Mosimane anajianda kutengeneza ufalme wake kwenye soka Barani Afrika ambapo anakwenda kuingoza klabu hiyo ya Misri kwenye fainali ya “TotalEnergies CAF Champions League” klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Athletic leo jumatatu kwenye dimba la Mohammed V Stadium.

Pitso Mosimane akili yake kwa sasa ni kuingoza klabu hiyo kubwa nchini misri na Afrika kuchukua ubingwa kwa mara ya tatu mfurulizo na mara 11 kwa ujumla, pia kocha huyo kutokea afrika kusini anaweza kuifikia rekodi ya Manuel Jose kwa kufanikiwa kushinda ubingwa wa Afrika mara nne.

Kocha huyo wa kireno Manuel Jose amefanikiwa kuchukua ubingwa wa afrika mara nne akiwa na klabu ya Ahly mwaka 2001, 2005, 2006 na 2008. Wakati Pitso Mosimane amechukua mara tatu mara ya kwanza akiwana na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini mwaka 2016 na mawili akiwa na Al Ahly.

“Ni heshima, na sifa kkwenye historia ya klabu yetu kufanikiwa kucheza fainali ya tatu mfurulizo sababu hatukuwai kufanya hivyo. Ijapokuwa tumecheza fainali nyingi sana lakini hatujawai kucheza fainali tatu mfululizo.

“Kwa jinsi ilivyo muhimu kwenye historia ya klabu, kiukweli hatuna shauku nayo, tunashauku na mchezo wenyewe,” Pitso Mosimane alisema kabla ya mchezo wa jumatatu.

Aliongeza, “kwa sababu nini maana ya kucheza fainali ya tatu mfurulizo na usishinde?, mtazamo wetu hauko hivyo, mtazamo wetu ni kushinda kombe. Bila shaka tunatambua kwamba tumefika fainali ya tatu mfurulizo na ni hatua kubwa kwa sababu hakuna timu iliyofanya hivyo.”

Pitso Mosimane akifanikiwa kuchukua ubingwa kwenye mchezo, ataweka kumbukumbu isiyofutika kuwa kocha wa kwanza kutoka Afrika kufanikiwa kuchukua ubingwa “TotalEnergies CAF Champions League” mara tatu mfurulizo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE....KITASA KIPYA CHA YANGA CHAFUNGUKA ISHU YA KUWEKWA BENCHI...