Habari za michezo

MORRISON ATHIBITISHA KURUDI TENA BONGO….YANGA WATAJWA KUWA NYUMA YA MCHEZO MZIMA….

admin June 1, 2022 1:36 pm


Aliekuwa mchezaji wa Simba SC, Bernard Morisson amethibitisha kurejea Tanzania hivi karibuni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram (Insta Story) Bernard Morrison amethibitisha kuwa yupo njiani kurejea Tanzania

Ikumbukwe kuwa nyota huyo alipewa mapumziko na Simba Sc pamoja na kuagwa/kutakiwa kila la heri katika maisha yake mapya ya soka.

Taarifa zinasema Morisson yuko mbioni kurejea Klabu yake ya zamani Yanga, na tayari ameshamalizana na matajiri wa Klabu hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Morrison kuichezea Yanga endapo dili hilo litafanikiwa ,ambapo anatazamiwa kuziba pengo lililoachwa wazi na Saido Ntibazonkiza ambaye naye ameshaagwa ndani ya Mabingwa hao watarajiwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.

TETESI ZA USAJILI BONGO: BAADA YA KUACHWA YANGA…NTIBAZONKIZA ATAJWA ‘KUNUKIA’ DTB FC…ISHU IKO HIVI.. JEMEDARI SAID:- WALIOFANYA USAJILI WA KINA PETER BANDA NA WENZAKE NDIO WALIOPASWA KUFUKUZWA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply