Habari za michezo

RASMI…SHOMARY KAPOMBE APIGWA CHINI TAIFA STARS….MWAIKENDA ALAMBA SHAVU…SABABU HIZI HAPA…

admin June 1, 2022 9:22 am


Beki wa Kulia wa Simba SC Shomari Kapombe ameondolewa kwenye kikosi Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika ‘AFCON 2023’.

Stars itacheza ugenini Juni 04 nchini Benin dhidi ya Niger, kisha itarejea nyumbani Dar es salaam kucheza dhidi ya Algeria Juni 08.

Kapombe ameondolewa kwenye kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na majeraha alioyapata katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold FC uliomalizika kwa sare ya 1-1 jijini Mwanza.

Maumivu hayo yalimfanya Kapombe kukosa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans uliochezwa Jumamosi (Mei 28), Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Tayari Benchi la Ufundi limeshafanya maamuzi ya kujaza nafasi ya Kapombe kwa kumwita Lusajo Mwaikenda wa Azam FC.

PAMOJA NA KUPOTEZA MATUMAINI YA KOMBE LOLOTE MSIMU HUU…MASTAA SIMBA WAPEWA ‘LIKIZO FUPI’…USAJILI WAJA… TETESI ZA USAJILI BONGO: BAADA YA KUACHWA YANGA…NTIBAZONKIZA ATAJWA ‘KUNUKIA’ DTB FC…ISHU IKO HIVI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply