Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA PASCAL WAWA KUSAJILIWA SINGIDA BIG STARS…..UKWELI WOTE UKO HIVI…

admin June 2, 2022 8:17 am


UONGOZI wa Singida Big Stars imeweka wazi kuwa unatambua ubora wa beki wa Simba, Pascal Wawa ila haina mpango wa kumsajili kwa muda huu.

Timu hiyo ambayo ilikuwa inaitwa DTB ilipokuwa inashiriki Championship inatajwa kuwa katika mazungumzo na Wawa ambaye mkataba wake unakaribia kuisha msimu utakapomeguka.

 Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars,Muhibu Kanu amesema kuwa mipango ya usajili ipo na watasajili wachezaji wazuri kwa malengo.

“Tuna mpango wa kufanya usajili mzuri kwa malengo kwa kutumia ripoti ya benchi la ufundi lakini suala la kumsajili Wawa, (Pascal) kwa sasa halipo kwenye mpango wetu.

“Mimi ninahusika kwenye masuala ya usajili hivyo ni suala la kusubiri ripoti inaeleza nini na inahitaji kitu gani kumbuka kwamba tumetoka kukamilisha kazi ya kupanda kutoka Championship na sasa tupo kwenye ligi lazima tujiandae,” amesema Kanu.

IMEFICHUKA…KUMBE PABLO HAKUTAKA CHAMA ASAJILIWE SIMBA….’KIBOSILE ALIMSAJILI KINGUVU KWA MAHABA YAKE.’.. BAADA YA KUWATEMA PABLO NA MORRISON…MO DEWJI ABARIKI CHAMA NA MASTAA HAWA10 KUPIGWA CHINI SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply