Habari za michezo

FAGIO LA CHUMA KUPITA NA MASTAA HAWA 14 NDANI YA YANGA…MANARA ATILIA MKAZO …MAKAMBO,NKANE NA CHICO NDANI…

admin June 3, 2022 2:29 am


Mastaa 14 ndani ya kikosi cha Yanga, wapo kwenye hesabu za kufyekwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2022/23.

Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema kuwa, usajili wa msimu ujao utakuwa ni mkubwa na wenye kuzingatia ripoti ya benchi la ufundi.

“Tuna malengo makubwa na tunajua wapi ambapo tulishindwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa tutasajili wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ili kuleta ushindani kimataifa,” alisema Manara.

Habari zinaeleza kuwa, miongoni mwa wachezaji ambao wataachwa moja kwa moja na wengine kutolewa kwa mkopo ni Erick Johore na Ramadhan Kabwili, hawa ni makipa hawajacheza hata mechi moja ya ligi msimu huu.

David Bryson, amecheza mechi 6, Abdallah Shaibu (mechi 1), Deus Kaseke (mechi 10) na Heritier Makambo (mechi 18), Yusuph Athuman (mechi 6), Yassin Mustapha (mechi 9), Paul Godfrey (mechi 1), Crispin Ngushi (mechi 3), Dennis Nkane (mechi 10), Balama Mapinduzi (mechi 1), Chico Ushindi (mechi 5) na Ibrahim Abdallah (mechi 2).

MAMBO YAZIDI KUFICHUKA SAKATA LA PABLO KUFUKUZWA SIMBA….KUMBE UGOMZI WAKE NA CHAMA ULIPELEKEA YOTE HAYA… PAMOJA NA KUCHECHEMEA MSIMU HUU…REKODI YA KAGERE BADO YADAI LIGI KUU…SI MPOLE WALA MAYELE ANAYEIWEZA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply