Home Habari za michezo KUHUSU KUWAACHA MZAMIRU NA ONYANGO….SIMBA WAIBUKA NA HILI TENA….AHMED ALLY AGUSIA YA...

KUHUSU KUWAACHA MZAMIRU NA ONYANGO….SIMBA WAIBUKA NA HILI TENA….AHMED ALLY AGUSIA YA MO DEWJI…

KLABU ya Simba imesema itaendelea kuwa na kiungo wake, Mzamiru Yassin kwa kumpa mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano mbalimbali ndani ya nje ya nchi na si miongoni mwa wachezaji ambao wataachwa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema ni kweli mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika, lakini atapewa mkataba mpya kutokana na kiwango chake na mchango mkubwa alioutoa kwenye klabu hiyo.

“Hivi sasa tunavyozungumza ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, unawezaje kumuacha mchezaji ambaye anaichezea timu ya taifa? Kama taifa linamwamini kwa nini isiwe sisi Simba,” alisema Ahmed akizima tetesi kuwa mchezaji huyo ni mmoja wa watakaoachwa msimu huu kutokana na maboresho makubwa yanayotarajiwa kufanyika ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

Meneja huyo alikiri kuwa wapo wachezaji ambao mikataba yao inaisha na muda si mrefu majina yao watayaweka hadharani na wataachana nao kwa wema kwa sababu wameifanyia Simba makubwa, lakini si kwa Mzamiru.

“Mzamiru ni mmoja wa wachezaji ambao nao mikataba yao inamalizika, lakini yeye atasalia, lakini wapo ambao inaisha, tutawapa mkono wa kwa heri kama ikithibitika hatuwezi kuendelea nao kwa sababu mbalimbali. Tumeshuhudia kauli kadhaa za Rais wetu wa Heshima Dk. Mohamed Dewji ‘Mo’ kuwa tunahitaji kufanya maboresho makubwa kwenye kila eneo, hivyo kuna watakaoondoka na watakaoingia, hivyo watu wa usajili ni lazima wawe makini ili tupate wachezaji sahihi wenye hadhi ya Simba,” alisema.

Kuhusu beki wa kati, Mkenya Joash Onyango, ambaye naye anamaliza mkataba, Ahmed alisema ni beki mzuri ambaye anastahili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Alibainisha kuwa kwa sasa kuna vikao vizito ndani ya klabu kwa ajili ya kusaka kocha, pia kufanya usajili bora na mkubwa ambao utawavusha kutoka hapo walipo kwenda kwenye hatua nzuri zaidi.

“Kikosi chetu kilirejea kambini Jumatatu na Jumanne kilianza mazoezi kujiandaa na mechi tano za kumalizia msimu,” alisema.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA MASHABIKI WA YANGA, ISHU IKO HIVI

Katika hatua nyingine, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa uongozi upo katika mazungumzo ya kuzinasa saini za nyota wawili akiwamo kiungo wa AC Horoya FC, Morlaye Sylla na mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole.

Simba ambao wameanza kufatilia baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kufanya kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao, kwa sasa wanahusishwa na kiungo huyo raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 23.

Taarifa za uhakika  kuhusu usajili ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa nyota huyo wameanza kumfuatilia pamoja na kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Mpole.

Lakini Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alipoulizwa kuhusu tetesi zilizozagaa, alisema wachezaji wanaotajwa ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu kila kitu kitawekwa wazi muda ukifika.