Habari za michezo

BAADA YA KUUKOSA UBINGWA WA KLABU BINGWA AFRIKA MSIMU HUU…RAIS AL AHLY ‘AIWASHIA MOTO’ CAF…

admin June 13, 2022 2:46 am


Rais wa club ya Al Ahly ya Misri Mahmoud El-Khatib ameweka wazi mtazamo wake na mapendekezo yake kwenda kwa Shirikisho la soka Afrika CAF kufuatia kupoteza kwa timu yake 2-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Mahmoud anaamini kuwa sasa ni wakati sahihi kwa CAF kurudisha mfumo wa zamani kwa kuchezwa kwa fainali mbili za nyumbani na ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu mfumo wa mchezo mmoja umefeli.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa Mahmoud zilizosababisha aseme mfumo huo umefeli ni kutokana na Afrika miundombinu ya kusafiri sio sawa na Ulaya na gharama yake iko juu kingine Afrika hawatumii noti moja kama Ulaya, matatizo ya mashabiki kupata visa.

Bibo ameyasema hayo baada ya fainali mbili za Ligi ya Mabingwa kuchezwa Morocco lakini pia mashabiki wengi wa Al Ahly walikwama kuingia Morocco sababu za masuala ya visa na usafiri pia

KUHUSU ISHU YA BWALYA KUTAKIWA NA AMAZULU FC YA AFRIKA KUSINI…UONGOZI SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA… SIMBA WAENDELEA KUIKIMBIZA YANGA MICHANGO YA NANI ZAIDI…BUMBULI ASHTUKIA ‘JANJA JANJA’ YA UPANDE WA PILI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply