Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUBEBA UBINGWA….MANARA AIBUKA NA HILI KUHUSU INJINIA HERSI…ADAI BILA YEYE HAKUNA KITU..

admin June 17, 2022 11:41 am


Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema Rais mtarajiwa wa klabu hiyo Injinia Hersi Said ndiyo mwamba aliyeleta mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kutoka na kujitoa kwake kuipambania Yanga katika kila hatua.

Manara amemmwagia Hersi sifa hizo wakati akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wake ambao ameupa jina la Mkutano wa kuhutubia Taifa hii ikiwa ni mara baada ya juzi klabu ya Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2021/2022.

Mbali na Hersi Manara pia amemshukuru Mfadhiri/Mdhamini wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa namna anavyojitoa katika kuisaidia klabu hiyo, sambamba na huyo amewapongeza wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi kwa kufanikisha kuisaidia timu hiyo kuchukua kombe la 28 la Ligi kuu Bara.

IMEISHA HIYOO…MORRISON NI YANGA TENA…AOMBA MSAMAHA SIMBA…MSUVA ‘AJIUZA’ MSIMBAZI,JANGWANI… MANARA AMLIPUA JEMEDARI SAIDI…ADAI ALIMSINGIZIA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KIPINDI CHA RAIS MAGUFULI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply