Habari za michezo

BAADA YA KUONA MAYELE ANASIFIWA SANA KILA KONA…MPOLE AVUNJA UKIMYA…AWACHANA WANASIFIA WAGENI…

admin June 18, 2022 4:17 pm


Straika wa Geita Gold, George Mpole amewataka Watanzania kuthamini wachezaji wazawa tofauti na wanavyowachukulia.

Akizungumza jana, Mpole alisema licha ya wao kutozungumzwa sana ila wanafanya kazi kubwa ingawa hawapewi sifa kama ambavyo wageni wamekuwa wakiimbwa kila siku.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kuthamini vya kwao sina maana wageni hawafanyi mambo makubwa ila mzani ni lazima ubalansi licha ya ukweli wenyewe tunajifunza kutoka kwao,” alisema na kuongeza;

“Siongei kwangu binafsi ila ni kwa wazawa wote, wapo ambao wanaonyesha uwezo mkubwa kuliko hata hao wageni ila kwa bahati mbaya tunawasahau na kuthamini vya nje jambo tunalopaswa kubadilika.”

Mpole ndiye kinara mzawa mwenye mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara. Nyota wa Yanga, Fiston Mayele anaongoza msimamo wa wafunga akiwa na mabao 16.

POGBA AIAGA MAN UNITED KWA ‘KICHAMBO CHA KIZARAMO’…ADAI ATAWAKOMESHA WAONE KUWA WALIMKOSEA… KUHUSU UFUNGAJI BORA MSIMU HUU…MAYELE AZIDI KUMTAMBIA MPOLE….”SIKUBALI KIRAHISI”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply