Habari za michezo

AZIZ KI, MORRISON WAIPA JEURI YANGA….MANARA ATUPA DONGO MSIMBAZI…ADAI UBORA WAO NI ROBO TU…

admin June 20, 2022 2:57 am


 Kuelekea msimu ujao wa 2022/23, Yanga wameanza kufanya maboresho ya kikosi chao, ambapo mpaka sasa wamekamilisha usajili na kumtangaza mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Lazarous Kambole.

Ukiachana na Kambole, mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu Bara wanatajwa kuwa tayari wamemalizana na mastaa wengine wakiwemo aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mmosas, Stephane Aziz Ki na kiungo wa Simba, Bernard Morrison.

kuhusu usajili wa kikosi chao, Msemaji wa Yanga, Haji Manara alisema: “Tayari tumeshaanza mchakato wa kufanya maboresho ya kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao na kupitia mapendekezo ya kocha Nabi (Nasreddine) tumeanza kutambulisha wachezaji wapya.

“Tumeweka wazi kuwa tutafanya usajili wa mastaa wanne au watano, niwahakikishie kuwa huu moto tulionao msimu huu ni robo tu ya ubora wa kikosi tutakachokuwa nacho msimu ujao, hivyo wapinzani wetu wajiandae.”

KOCHA MPYA SIMBA NI HUYU HAPA…STRAIKA MWINGINE ASAINI KIMYA KIMYA…NABI AMVUTA MSUVA YANGA… BEKI KISIKI AGOMEA MKATABA MPYA SIMBA…AITAJA COAST UNON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply