Azam FC

Azam FC Yaanza Mazungumzo na Aidan Rasmos wa Coastal Union

Vardo June 30, 2026 12:50 pm

KATIKA harakati za kuimarisha kikosi kuelekea msimu wa 2026/27, Azam FC imeanza mazungumzo ya kumuwania beki wa kushoto wa Coastal Union, Aidan Rasmos, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuongeza ushindani kikosini.

Baada ya kumaliza msimu uliopita bila kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam imeingia sokoni kutafuta wachezaji wapya kwa mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Florent Ibenge, likiwa na lengo la kujenga kikosi kitakachoshindania mataji msimu ujao.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya Azam FC na upande wa mchezaji tayari yameanza,Rasmos anaonekana kuwa chaguo muhimu la kuziba nafasi inayotarajiwa kuachwa na beki wa kushoto Nathaniel Chilambo, ambaye anahusishwa na uwezekano wa kujiunga na Simba mwishoni mwa msimu huu.

Rasmos amekuwa mmoja wa mabeki waliovutia zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kiwango bora alichokionyesha akiwa na Coastal Union.

Uwezo wake wa kucheza kwa kasi, kupanda kushambulia na kurejea kwa haraka kwenye majukumu ya ulinzi umemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na klabu kadhaa.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mazungumzo hayo, Azam inaona usajili wa Rasmos unaweza kuongeza ushindani katika safu ya ulinzi na kuimarisha kikosi kuelekea msimu wenye ratiba ngumu.

“Azam inahitaji kuongeza nguvu katika eneo la beki wa kushoto ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushindania ubingwa wa ligi pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

Hersi Asalia Bila Mpinzani, Muhula Mwingine Wanukia Yanga Ivory Coast Dhidi ya Norway Watafuta Kuvunja Rekodi