SHIRIKISHO la soka Africa CAF limethibitisha kurejea kwa tuzo za CAF 2022 ambapo zitafanyika nchini Morocco Julai 21, 2022 huku wakiaznisha kipengele kipya cha mchezaji bora wa mwaka wa klabu za Interclub.
Tuzo hizo zitaandaliwa kabla ya fainali ya mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake Morocco 20223 iliyopangwa kufanyika kati ya 02 Julai – 23 Julai 2022.
Tukio hilo pia litaambatana na kumbukumbu ya miaka miwili ya kuzinduliwa kwa mkakati wa mpira wa miguu kwa Wanawake CAF.
Sambamba na hilo, kipengele cha mchezaji bora wa mwaka wa klabu za Interclub imetambulishwa kufuatia kuanzishwa kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF ya TotalEnergies CAF mnamo Novemba 2021.
Vitengo vingine ni pamoja na Mchezaji Bora wa klabu ya Interclub, mchezaji bora chipukizi wa mwaka, Timu ya taifa ya mwaka, Kocha bora wa mwaka, Klabu bora ya mwaka, Bao bora la mwaka.
Washindi wataamuliwa kwa kura kutoka kwa manahodha na makocha wa vyama wanachama, Waandishi wa habari waliochaguliwa, Kikundi cha utafiti wa ufundi cha CAF na wakongwe wa CAF.
Mshambulizi wa Senegal Sadio Mane na Asisat Oshoala wa Nigeria walitwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa Wanaume na Wanawake msimu uliopita.