Home Habari za michezo KISA TETESI ZA MNIGERIA WAO AKPAN KUJIUNGA NA SIMBA…COASTAL UNION WAIBUKA NA...

KISA TETESI ZA MNIGERIA WAO AKPAN KUJIUNGA NA SIMBA…COASTAL UNION WAIBUKA NA MADAI HAYA MAPYA…


BAADA ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kiungo tegemeo wa Coastal Union, Mnigeria Victor Akpan, tayari amesajiliwa na Klabu ya Simba kuelekea msimu mpya wa 2022/23, Kocha Mkuu wa ‘Wagosi wa Kaya’ hao, Juma Mgunda, alisema hakuna geni katika suala hilo kwa kuwa ni jambo la kawaida.

Simba ipo katika mkakati mzito wa kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao kutokana na msimu huu kupoteza mataji yake matatu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga; ambayo ilianza msimu kwa kuipokonya Ngao ya Jamii, kisha ikainyang’anya ubingwa wa Ligi Kuu Bara na sasa inaelekea fainali ya Kombe la FA baada ya kuwatupa nje mahasimu wao hao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka mjini Lindi ambapo Coastal Union leo, Jumatatu inacheza na Namungo FC kwenye mechi ya Ligi Kuu, alisema yeye pia anazisikia habari hizo za Akpan kumalizana na Simba, lakini hayo ni mambo ya kawaida kwenye timu na ana haki ya kufanya hivyo.

“Hizo habari zipo na ni za kawaida kwenye timu kwa kipindi hiki, kama inatokea hivyo basi ni haki yake, lakini Akpan huku tunaye kwa ajili ya maandalizi ya kucheza na Namungo FC kesho (leo),” alisema.

Akpan ambaye amekuwa ni moja ya wachezaji wenye msaada mkubwa ndani ya kikosi cha Wagosi wa Kaya ambapo kwenye mechi iliyopita dhidi ya Yanga licha ya kufungwa mabao 3-0 yeye pamoja na Abdul Hamisi Selemani ” Sopu” walikuwa kivutio kwa kuichezesha timu vizuri.

Mwishoni mwa wiki iliyopita taarifa zilienea kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa kiungo huyo amesaini mkataba wa kuitumikia Simba msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.

Taarifa hizo zilizidi kufafanua kuwa Coastal Union imeridhia kumwachia kiungo huyo kwenda Simba kwa dau la shilingi milioni 100.

SOMA NA HII  WAKATI MAMBO YAKIZIDI KUWA MAMBO...BOCCO AVUNJA UKIMYA SIMBA...ADAI SIKU ZA MWANZO NI TOFAUTI NA SASA...