Habari za michezo

MASTAA WALIOIPAMBANIA DTB MPAKA IKAPANDA LIGI KUU WATEMWA WOTE…WABLOKIWA MPAKA WHATSAPP…

admin June 23, 2022 3:26 am


Uongozi wa timu mpya kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao, Singida Big Stars (zamani DTB) ‘umewaleftisha’ mastaa wake kibao walioipandisha daraja timu hiyo na kuanza kusuka upya chama hilo.

Taarifaza kuaminika zinasema Singida imeachana na robo tatu ya wachezaji wake waliokuwepo msimu huu na kubakiza wasiozidi 10 na sasa imeanza kusajili wengine wapya.

Taarifa za kuaminika tayari nyota hao wakiongozwa na Yanick Bazora, Yusuph Mlipili, David Mwantika, Majaliwa Shaban na Tafdazwa Kutinyu, Majaliwa Shaban James Msuva na wengine wengi wamepewa barua za kuachana na timu hiyo sambamba na kuleftishwa kwenye magrupu yote ya ‘Whatsapp’ ya timu hiyo.

Moja ya wachezaji kati ya hao walioleftishwa ambaye hakuwa tayari jina lake kuwekwa wazi, amelalamika kuwa uamuzi huo umekuwa ghafla lakini hawana budi kukubali.

“Ndivyo maisha ya soka yalivyo, ghafla tu tumetolewa kwenye magrupu ya timu na kuagwa hivyo hatutokuwa ndani ya timu ile msimu ujao,” alisema nyota huyo na kuongeza;

“Wakati timu inapanda tuliambiwa tutakaa mezani kuzungumza mikataba mipya kwa ajili ya msimu mpya Ligi Kuu, lakini wakati tunasikilizia kuitwa ndio imetokea hivyo tumeachwa.”

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Muhibu Kanu alieleza timu hiyo kila jambo inalofanya imezingatia matakwa ya viongozi wa timu na kuhusu wachezaji ni kulingana na ripoti ya benchi la ufundi.

“Kila kitu tunakifanya kwa ubora, kwa wachezaji watabaki wale waliopendekezwa na benchi la ufundi na wengine tutaachana nao kwa wema pia tutasajili wengine ili kuwa na timu yenye ushindani kwenye ligi,” alisema Kanu.

A-Z JINSI FEI TOTO ALIPODHIHIRISHA THAMANI YAKE YA BILIONI MOJA JANA…CHIKO USHINDI AMTIMULIA VUMBI MAYELE… HUU HAPA UKWELI WOTE KWA NINI KYOMBO ALITAMBULISHWA SINGIDA BIG STARS WAKATI ALISHASAINI MKATABA NA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply