Habari za michezo

BAADA YA KUONA HALI HALISI ILIVYO…ERASTO NYONI NAYE ASHUKURU MASHABIKI SIMBA…”TULIANZA NA TUNAMALIZA WOTE”…

admin June 24, 2022 3:28 am


Beki wa Simba, Erasto Nyoni amewashukuru mashabiki wao kwa namna walivyowapa sapoti licha ya kwamba wameshindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu huu.

Yanga tayari wametangazwa mabingwa wapya wa ligi hiyo huku wakisubiri pia kucheza mechi ya fainali ya ASFC dhidi ya Coastal Union inayotarajiwa kuchezwa Julai 2, mwaka huu jijini Arusha.

Simba msimu huu umekuwa mbaya kwao kutokana na kupoteza makombe yote muhimu la Ngao ya Jamii, Ligi Kuu sambamba na la ASFC.

Nyoni alisema, juhudi ambazo wachezaji uzifanya katika timu mashabiki wanachangia kwa hali kubwa chachu ya mafanikio ya timu yao na msimu huu wameanguka wote. “Mashabiki wetu ni watu muhimu sana na wa kipekee, tulianza pamoja tunamaliza pamoja ni jambo la kujivunia sana, kupoteza makombe kila mwanasimba kaumia lakini ndio mpira,” alisema Nyoni.

Alisema wanajitahidi michezo iliyobaki wapate matokeo mazuri licha ya kushindwa kuchukua taji hilo mara tano mfululizo.

Simba imebakiza kucheza na , Prisons (Sokoine) na Mbeya Kwanza (Majimaji).

A-Z JINSI MASHABIKI WALIVYOMUAGA WAWA JANA…AMIMINIWA MAPESA KILA KONA YA UWANJA…NDEMLA AFANYA KITUKO… KISA SIMBA KUMZUIA MORRISON…YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…BUMBULI AIBUKA NA KUJIBU MAPIGO…”IWE ISIWE TUTAMSAJILI”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply