Habari za michezo

KOMBE LA YANGA DAR..:MANARA NA SENZO WASHUKA KLABU YA SIMBA NA KOMBE…MASHABIKI WAWACHANGAMKIA CHAP…

admin June 26, 2022 1:23 pm


Mabosi wa Yanga Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wameshuka mtaa wa Msimbazi Kariakoo kuwatambia waajiri wao wa zamani.

Basi lililobeba wachezaji lilipofika Msimbazi Manara aliamuru lisimame kwa dakika kadhaa akitaka kushuka na akashuka sambamba na Senzo.

Wawili hao wameshuka huku wakishika kombe lao la ligi kisha kupiga nao picha katikati ya barabara huku wakishangiliwa na maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo.

Baada ya dakika tatu Manara na Senzo ambao wameingia Yanga wakitokea Simba waliliinua kombe hilo juu huku wakishangiliwa na kurudi ndani ya basi hilo maalum.

Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Senzo na Manara tangu wakutane Yanga wakitokea Simba ambapo mara ya mwisho kushangilia ubingwa huo walikuwa ndani ya Simba.

COASTAL UNION WACHOMOZA MSAFARA WA KOMBE LA YANGA LEO…WAIMBWA KILA KONA YA JIJI…MASHABIKI HAWAELEWI KITU… MASHABIKI SIMBA WAJIBU MAPIGO YA YANGA KARIAKOO LEO…WATOA NNJE MAKOMBE YAO YOTE…YANGA WAKIMBIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply