Habari za michezo

COASTAL UNION WACHOMOZA MSAFARA WA KOMBE LA YANGA LEO…WAIMBWA KILA KONA YA JIJI…MASHABIKI HAWAELEWI KITU…

admin June 26, 2022 1:09 pm


Bado Coastal …bado Coastal…bado Coastal’, hivi ndivyo mashabiki wa Yanga wakiimba wakati wakipokea taji lao la ligi.

Mashabiki hao wameipiga mkwara Coastal Union wakati wakiwa kwenye msafara wa kupokea kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Yanga imerejea asubuhi ya leo ikitokea jijini Mbeya ambapo wamekabidhiwa rasmi kombe hilo baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mashabiki hao wakiwa wanakimbia barabarani kupokea kombe hilo wamekuwa wakiimba nyimbo wakidai bado Coastal Union.

Nyimbo hiyo ni sawa na kuipiga mkwara Coastal Union ambao watakutana nao Julai 2, kwenye Fainali ya Kombe la Azam Shirikisho.

Mchezo huo ambao utapigwa jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Yanga itakuwa inawania taji la tatu msimu huu.

Msimu huu tayari Yanga imeshachukua mataji mawili ya Tanzania bara wakitangulia kuchukua Ngao ya Jamii baada ya kuwachapa Simba,kisha jana kuchukua lile la ligi.

MASHABIKI YANGA WAISIMAMISHA DAR….KISHONDO CHAKE SIMBA WAKASOME AISEE…GSM AWA HABARI YA MJINI… KOMBE LA YANGA DAR..:MANARA NA SENZO WASHUKA KLABU YA SIMBA NA KOMBE…MASHABIKI  WAWACHANGAMKIA CHAP…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply