Habari za michezo

MASHABIKI YANGA WAISIMAMISHA DAR….KISHONDO CHAKE SIMBA WAKASOME AISEE…GSM AWA HABARI YA MJINI…

admin June 26, 2022 1:04 pm


Nyomi ya mashabiki waliojitokeza kuipokea Yanga ambayo inasindikizwa na eskoti ya Polisi imefunga njia na kusababisha foleni kubwa barabara zote.

Yanga tayari wameshatoka uwanja wa ndege wanaelekea Jangwani wakipita mtaa wa Msimbazi na shughuli hiyo imesababisha foleni upande wa barabara inayoenda Gongo la Mboto na mjini.

Mashabiki wa timu hiyo wanaongozana na msafara wa timu huku wakiimba bila kuchoka GSM na kutaja jina la Fiston Mayele na kushangilia staili yake ya kutetema.

Polisi wanaongoza msafara pia hawapo nyuma kwa kukimbizana na msafara kuhamasisha mashabiki waondoke barabarani ili msafara uwahi kufika eneo la tukio.

DILI LA MSUVA KUTUA YANGA SI MCHEZO AISEE…GSM WAMWEKEA MEZANI MIL 350…NABI APAGAWA KWA MAVITU YAKE… COASTAL UNION WACHOMOZA MSAFARA WA KOMBE LA YANGA LEO…WAIMBWA KILA KONA YA JIJI…MASHABIKI HAWAELEWI KITU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply