Kocha mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema wana kila sababu ya kuchukua pointi tatu katika mchezo wao wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Yanga wataikaribisha Mtibwa kesho katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu huu utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Waandishu wa habari, Nabi alisema anatambua ugumu wa wapinzani wao hakini wamejiandaa kuondoka na pointi tatu licha ya kuwa kombe la msimu huu tayari liko kabatini.
“Mtibwa Sugar sio timu ya kawaida wapo vizuri na wanasumbua timu nyingi, tumejiandaa kuchukua pointi tatu katika mchezo huu”. amesema Nabi.
Nabi amesema kwenye mchezo huo kunaweza kuwa na mabadiliko kwa kiasi kikubwa kutokana na baadhi wa wachazaji kuwa na kadi tatu za njano huku wengine wakiwa majeruhi.
“Kutakuwa na mabadiliko kesho kutokana na hali halisi ya kikosi chetu ambacho wachezaji nane wa kikosi cha kwanza wanaweza kuhukosa mchezo huo lakini nitaangalia dakika za kuwapatia vijana katika mchezo huu”. amesema Nabi na kuongeza;
“Changamoto kubwa kwetu ni kuwa tuna mechi nyingine muhimu ya fainali ya kombe la Shirikisho ambapo mchezo huo utatuhiataji tuwe na kikosi kamili hivyo katika mchezo wa kesho msishangae kuona mabadiliko makubwa”.