WAKATI homa ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi hii ikizidi kupamba moto jijini hapa kiingilio cha chini katika mchezo huo imetajwa kuwa ni shilingi elfu 10,000.
Mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na ubora wa vikosi vyote utapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa jijini Arusha ambapo Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema viingilio VIP A itakuwa ni Sh 30,000,VIP B Sh20,00 huku mzunguko ukiwa ni Sh10,000.
Kuhusu VVIP amesema itakuwa ni maalum kwa ajili ya mwaliko huku akiwataka wale wote ambao wanaweza kukaa katika eneo hilo kuwasiliana na TFF hili kuweza kupata mwaliko.
Ametaja maeneo ambayo tiketi zinapatikana kuwa ni TTCL makao makuu, pamoja na uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku akiongeza kuwa siku ya mchezo wenyewe tiketi hizo hazitopatikana uwanjani hapo lakini zitauzwa katika maeneo jirani na hapo pamoja na Kilombero na Sanawari.
“Muda wa mechi ni saa 9:00 alasiri na haitoruhusiwa gari yoyote uwanjani tofauti na ile ya wagongwa kikubwa pia mashabiki wazinganite muda wa kufungua mageti ambayo ni saa 4:00 asubuhi” amesema Ndimbo.
Kuhusu maandalizi ya mchezo amesema kila kitu kiko sawa kuanzia uwanjani pamoja na sehemu ya kucheza (pitch),ambayo imefanyiwa maboresho makubwa kuendana na hadhi ya mchezo wenyewe.
Yanga imetinga fainali baada ya kuichapa Simba goli 1-0 kwenye nusu fainali huku Coastal Union FC ikiifunga Azam FC 6-5 kwenye mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kukamilika bila timu hizo kufungana.