Home Habari za michezo BAADA YA KUWATEMA PABLO NA MORRISON…MO DEWJI ABARIKI CHAMA NA MASTAA HAWA10...

BAADA YA KUWATEMA PABLO NA MORRISON…MO DEWJI ABARIKI CHAMA NA MASTAA HAWA10 KUPIGWA CHINI SIMBA…


Simba imemtema Bernard Morrison. Ikatema Kombe la FA. Imemtema Kocha Pablo Franco. Inaelekea kutema ubingwa wa Ligi. Na inakwenda kutema mastaa kibao. Pape Ousmane Sakho yumo ndani.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba ni kwamba Sakho na Peter Banda watauzwa muda wowote kuanzia sasa kama ilivyofanyika kwa Rally Bwalwa anayekwenda Amazulu ya Sauzi.

Wengine wanaokwenda na maji ni mkongwe Meddie Kagere, Pascal Wawa, Taddeo Lwanga, Chris Mugalu na kiraka Erasto Nyoni. Kwenye orodha hiyo ya wanaotemwa yupo pia Gadiel Michael ambaye anaenda Singida Big Stars (zamani DTB) na Bernard Morrison ambaye tayari alishamwagwa.

Joash Onyango kama ataendelea kushinikiza kupewa dau refu na mshahara mkubwa ili asaini mkataba mpya kwani huu wa sasa umeisha, naye pia atatemwa kwani uongozi hauko tayari kufanya hivyo haswa kutokana na umri wake. Inasemekana anataka zaidi ya Sh100 milioni kama ada ya kusaini.

Clatous Chama ambaye amerejea Simba hivi karibuni ana asilimia kubwa ya kuuzwa kama ikipatikana timu itakayofika dau huku baadhi ya klabu za Afrika Kusini zikitajwa.

Habari za uhakika zinataja wachezaji walioko salama na baadhi yao watakaoongezewa mikataba kuwa ni Henock Inonga, Jonas Mkude, John

Bocco, Aishi Manula, Mzamiru Yassin, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Beno Kakolanya.

Wengine wanaopewa nafasi kubwa ya kubaki ni Sadio Kanoute, Kennedy Juma, Kibu Denis, Israel Patrick Mwenda, Hassan Dilunga,Yusuf Mhilu, Jimmyson Mwanuke na kipa wa benchi Ally Salim.

PABLO SIKU 203

Safari iliyojaa misukosuko mingi na nyakati chache za furaha kwa kocha Pablo Franco ndani ya Simba imefikia tamati jana baada ya siku 203 tu alizoitumikia timu hiyo.

Uongozi wa Simba juzi ulitangaza rasmi kumfuta kazi Pablo na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes na kuliacha jukumu la kusimamia benchi la ufundi kwa kocha msaidizi, Selemani Matola.

“Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco Martin. Katika kipindi chake Pablo ametuwezesha kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.”

“Uongozi unamshukuru Pablo kwa mchango wake mkubwa ndani ya timu ambapo baada ya kuondoka kikosi kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola. Wakati huo huo, tumefikia makubaliano ya pande zote ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo, Daniel De Castro Reyes. Simba inawatakia kila kheri kocha Pablo na mtaalam wa viungo Daniel Castro katika majukumu yao mapya,” ilisema taarifa ya Simba.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUKAZIWA NA NAMUNGO JANA....PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AWATAJA WALIO ZINGUA...

Ilikuwa lazima ang’oke

Kulikuwa na sababu nyingi ambazo zilionyesha ishara ya wazi kuwa Pablo asingekuwa na maisha marefu ndani ya Simba ambazo baadhi zilitokana na makosa yake mwenyewe na nyingine hakuhusika nazo.

Kutokuwa na muendelezo wa kiwango bora cha kitimu ndani ya uwanja, kushindwa kuimarisha kiwango cha mchezaji mmojammoja, kutodhibiti nidhamu ya timu na mpasuko ndani ya kikosi uliosababisha hamasa na morali ya wachezaji kupungua siku hadi siku, ni matatizo ambayo yalionekana yangefupisha safari ya Pablo ndani ya Simba.

Ilionekana wazi Pablo na benchi lake la ufundi walishindwa kushughulikia changamoto hizo ndani ya timu na badala yake mara kwa mara kocha huyo alisimama hadharani na kutoa kauli za kukosoa yaliyokuwa yakijiri wakati yeye kama mkuu wa benchi la ufundi ndio alipaswa kuwa wa kwanza kuyashughulikia.

Lakini ukiondoa hayo, Pablo aliangushwa pia na mchango duni wa baadhi ya wachezaji kikosini hasa wale tegemeo na hata pia wale wapya waliosajiliwa walichangia kumpa wakati mgumu Pablo katika kutimiza malengo ambayo klabu iliyojiwekea.

Changamoto nyingine ambayo imemuangusha Pablo ni majeraha ya mara kwa mara ambayo wachezaji wake wamekuwa wakiyapata msimu huu jambo ambalo limefanya kusiwe na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi.

Uongozi Simba ujitazame

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Kassim Dewji kupitia kituo cha redio cha EFM, alisema kuwa kuna udhaifu wa kiuongozi ndani ya klabu hiyo unaochangiwa na utendaji usioridhisha.

ìWaajiriwa wengi Simba SC hawana taaluma ya ajira zao. Bodi haina nguvu ya kuwawajibisha waajiriwa wao,î alinukuliwa Dewji.

Kabla ya hapo, mwekezaji na Rais wa heshima wa Simba, Mohammed Dewji alisema kuwa klabu hiyo inapaswa kuchukua uamuzi mgumu kutokana na kufanya vibaya msimu huu.

“Huu umekuwa ni msimu mbaya zaidi kwa Simba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Bodi inatakiwa kuchukua uamuzi mgumu ili twende mbele. Tunatakiwa kufanyia marekebisho timu na mipango. Tumekosa hamasa, kiu na njaa ya kushinda mataji mwaka huu,” alisema Dewji.

Ikumbukwe juzi, mjumbe mwingine wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Mwina Kaduguda alisikika akimtetea kocha Pablo kupitia mahojiano yake na kituo kimoja cha redio akidai uamuzi wa kumtimua ni kumuonea huku akiita wawekezaji zaidi wajitokeze Simba ili kumsaidia Mohammed ‘Mo’ Dewji.