Home Geita Gold FC WAKATI YANGA WAKISEREBUKA NA UBINGWA WAO…GEITA GOLD WAMALIZA MSIMU KWA STAILI HII…

WAKATI YANGA WAKISEREBUKA NA UBINGWA WAO…GEITA GOLD WAMALIZA MSIMU KWA STAILI HII…


Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ ametamba kufikia malengo yake msimu huu baada ya kuihakikishia timu yake kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Geita ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 45, moja pungufu ya ilizonzo Azam inayokamata nafasi ya tatu.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, inasubiri kuona Azam itavuna nini katika mechi yao ya mwisho ili kuipata tiketi ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho la Afrika na kocha Minziro alisema anashukuru kuona wamemaliza ndani ya Nne Bora.

Akizungumza Kocha Minziro ameeleza kufikia malengo yake msimu huu na kuweka wazi haikuwa rahisi huku akiwapongeza viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Geita kwa ushirikiano.

“Naweza kusema imeisha kwani tayari tumefanikiwa kuwa kwenye malengo yetu ya kumaliza ndani ya Top 4. Mechi ijayo tutakuwa ugenini, tunahitaji kufanya vizuri na ikiwezekana tutamaliza nafasi ya tatu,” alisema Minziro na kuongeza;

“Haikuwa rahisi ligi ya msimu huu ilikuwa ngumu sana, tulianza kwa kusuasua lakini baadaye tukawa imara na hadi sasa tuko vizuri. Hii haijaja kwa bahati mbaya bali mipango na ushirikiano wa kila mtu ndani ya timu kwa ujumla.”

Katika mechi 29 ilizocheza hadi sasa ikisaliwa na moja kumaliza msimu huu wa ligi, Geita imeshinda mechi 12 sare tisa na kupoteza nane na kuvuna alama 45, ikiwa ni timu ya tatu kupoteza mechi chache baada ya Yanga ambayo haijapoteza hadi sasa na Simba iliyopoteza mara tatu.

SOMA NA HII  YANGA WANAPOMKATAA KISINDA LEO HUKU WAKITAKA MUJIZA YA USAJILI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here