Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….NABI AUNGURUMA KAMA SIMBA…ATOA AHADI YA KICHAPO CHA “MBWA...

KUELEKEA MECHI YA KESHO….NABI AUNGURUMA KAMA SIMBA…ATOA AHADI YA KICHAPO CHA “MBWA KOKO” KWA COASTAL..


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, amesema anauheshimu mchezo wa Fainali na kesho kikosi chake kitacheza kwa tahadhari kubwa dhidi ya Coastal Union.

Miamba hiyo itacheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kesho Jumamosi (Julai 02) katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, huku kila upande ukiamini unakwenda kuibuka mabingwa wa Michuano hiyo msimu huu 2021/22.

Kocha Mkuu wa Young Africans amezungumza na Waandishi wa Habari mjini Arusha na kueleza mipango na mikakati ya kuelekea mchezo huo, huku akionyesha kuwa makini na kuwaheshimu Coastal Union ambayo ameshaifunga mara mbili, katika Ligi Kuu msimu huu.

Amesema mchezo wa Fainali siku zote umekua na matokeo tofauti na michezo ya Ligi, hivyo atahakikisha wachezaji wake wanacheza kwa nidhamu kubwa, ili kufikia lengo la kumaliza kwa furaha ya kuwa mabingwa.

“Mchezo wa Fainali ni tofauti, tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na tahadhari kubwa, tunaamini wapinzani wetu wapo katika hali nzuri ya kupambana, hasa baada ya kupoteza dhidi yetu katika michezo ya Ligi Kuu,”

“Ninaamini mchezo utakua mzuri na wenye changamoto nyingi za ushindani, kikubwa ninawaombea wachezaji wangu waendelee kuwa salama hadi kesho siku ya mchezo, ili tupambane kwa lengo la kushinda mchezo wetu wa Fainali.” Amesema Kocha Nabi

Young Africans ilitinga hatua ya Fainali kwa kuichapa Simba SC 1-0, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Mei 28, huku Azam FC ikitupwa nje ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arudha Mei 29.  

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA LIGI KIBABE....UDHAIFU WA SIMBA HUU HAPA....'CHEZAJI LA CAF' LAWAUMBUA...