Home Habari za michezo BAADA YA TETESI ZA KUACHANA NA SIMBA KUZAGAA JUZI NA JANA…BARBARA AVUNJA...

BAADA YA TETESI ZA KUACHANA NA SIMBA KUZAGAA JUZI NA JANA…BARBARA AVUNJA UKIMYA…ADAI CHANGAMOTO NI…


MASHABIKI wa Simba walishaingiwa ubaridi baada ya mitandao ya kijamii kuanika kuwa Mtendaji Mkuu wa Barbara Gonzalez ameachia ngazi, lakini mwenyewe amevunja ukimya na kusisitiza yupo sana Msimbazi licha ya changamoto anazopitia.

Usiku wa juzi kupitia kurasa za mitandao ya klabu hiyo iliweka taarifa kuna ujumbe utakazungumzwa na Barbara ila baada walieleza jambo hilo limeshindikana.

Barbara alisema alikuwa anataka kushukuru, kuzungumza na mashabiki wa Simba kuhusiana na mambo mengi muhimu yaliyotokea kwenye klabu msimu uliopita pamoja na mipango yao ya msimu ujao.

Jambo hilo lilishindikana kufanyika kutokana mambo ya ndani kwenye klabu yalikwenda tofauti kama vile alivyokuwa akitarajia hadi morali na hali yake ya kupambana kwa ajili ya timu ilishuka.

Barbara alisema hakuwa kwenye hali nzuri wakati aliyotakiwa kuzungumza masuala ya timu kutokana na mambo fulani ya ndani hayakwenda kama vile alivyokusudia lililomfanya morali yake kushuka.

“Niweke wazi kwa sasa siwezi kuondoka wala kufikiria kuacha kazi yangu hii bado nipo nipo naendelea na majukumu ya kazi kwani changamoto ni sehemu ya safari katika mafanikio,” alisema Barbara na kuongeza

“Bado nipo Simba na naendelea kufanya majukumu yangu ya kila siku na niwambie  (jana saa 5:30 asubuhi) nipo njiani kwenda Airport, nasafiri nje ya nchi, kwa shughuli muhimu ya klabu yetu.”

SOMA NA HII  MECHI SABA ZAMPA MTU MILIONI 14 MERIDIAN BET