Mfungaji Bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Azam (ASFC), Abdul Hamis ‘Sopu’, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-trick kwenye fainali hizo baada ya kuwafunga Yanga kwenye sare ya mabao 3-3 akiwa na Coastal Union.
Sopu alianza kufunga dakika ya 11 kisha akafunga bao la pili dakika ya 88 kabla ya kufunga bao la tatu dakika ya 98 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Fainali imemalizika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa Coastal Union kupoteza kwa penalti 4-1 baada ya kumalizika dakika 120 wakifungana 3-3.
Wachezaji wengine wanamfuata kwa ufungaji katika mashindano hayo ni Heritier Makambo mabao saba, Elia Chibule wa Tunduru Korosho mabao matano, Iddi Kipagwile wa Azam FC mwenye mabao manne sawa naClatous Chama wa Simba.