Geita Gold FC

KUHUSU MPOLE KUJIUNGA NA SIMBA AU YANGA..MINZIRO KINYOONGEE AIBUKA NA KAULI HII YA HUZUNI…

admin July 3, 2022 3:09 am


Kocha Mkuu wa kikosi cha Geita Gold, Fred Felix Minziro, ameweka wazi kuwa ni kweli kuna uwezekano mkubwa wakampoteza straika na nahodha wa kikosi chao, George Mpole ambaye anatajwa kupokea ofa kutoka klabu za Simba na Yanga.

Mpole amekuwa miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye nafasi kubwa ya kuondoka ndani ya kikosi cha Geita Gold kutokana na uwezo mkubwa ambao ameuonyesha msimu huu akifanikiwa kuhusika katika mabao 21 katika michezo 30 ya Ligi Kuu aliyocheza msimu huu, akifunga mabao 17 na kuasisti mara nne.

Mpole ambaye alijiunga na Geita Gold akitokea Polisi Tanzania msimu uliopita, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Geita Gold, unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao, na tayari Simba na Yanga zimefanya mazungumzo naye huku pia akiwa na ofa kutoka nje ya nchi.

Kocha Minziro, alisema: β€œNi jambo lililo wazi kuwa tuko katika nafasi kubwa ya kumpoteza Mpole kuelekea msimu ujao kutokana na kile ambacho amekionyesha msimu huu, tunatamani kubaki naye, nami binafsi nimefanya mazungumzo naye kuona uwezekano wa kumbakisha.

β€œLakini kama mchezaji naye anatafuta maisha hivyo anaweza kufanya uchaguzi ambao anaona unamfaa, nasi tumejiandaa kwa chochote ambacho kitatokea.”

DEAL DONE….MKANDARA AKAMILISHA SAFARI YAKE YA KUTUA AZAM FC….SASA MAMBO NI ‘BULIBULI’…. KISA KUZOZANA NA KARIA….TFF WAMFUNGULIA SHAURI LA KESI MANARA…AKUMBUSHWA KANUNI ZA KUZINGATIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply