Habari za michezo

KISA KUZOZANA NA KARIA….TFF WAMFUNGULIA SHAURI LA KESI MANARA…AKUMBUSHWA KANUNI ZA KUZINGATIA…

admin July 3, 2022 10:16 am


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefungua shauri mbele ya Kamati ya Maadili dhidi ya ofisa wa klabu ya Yanga, Haji Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

Kamati ya Maadili kupitia kwa Mwenyekiti wake tayari imepewa taarifa kuhusu malalamiko dhidi ya Manara, hivyo itapanga siku ya kusikiliza shauri hilo na Mlalamikiwa atapewa taarifa.

TFF inawakumbusha wanafamilia ya mpira wa miguu kuwa wanabanwa na Katiba na Kanuni mbalimbali za mchezo huo, hivyo wanatakiwa kuwa makini kwa vitendo na kauli zao kuhusu mpira wa miguu.

Taarifa hii imekuja baada ya jana kuonekana Haji Manara akizozana na Rais wa TFF Wallace Karia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume, katika fainali ya ASFC 2022 kati ya Yanga na Coastal Union.

KUHUSU MPOLE KUJIUNGA NA SIMBA AU YANGA..MINZIRO KINYOONGEE AIBUKA NA KAULI HII YA HUZUNI… UKWELI MCHUNGU….KILICHOIGHARIMU SIMBA MSIMU HUU NI PAMOJA NA HAYA….CHAMA, BOCCO NA UONGOZI WAHUSIKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply