Habar za Usajili Simba

ACHANA NA UTAMBULISHO WA AKPAN LEO…MASTAA HAWA HAPA WANAFUATA KUTUA MSIMBAZI…HAKIKISHA UNABANDO…

admin July 10, 2022 11:31 am


Klabu ya Simba imenasa saini ya kiungo Mnigeria, Victor Akpan kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika timu ya Coastal Union.

Nyota huyo aliyeonyesha kiwango kizuri msimu ulioisha unakuwa ni usajili wa pili kwa wachezaji wakigeni ndani ya timu hiyo baada ya hapo awali kutambulishwa Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia.

Simba chini ya Kocha mpya, Zoran Maki inaendelea kuboresha kikosi chake kwa ajili ya michuano mbalimbali ya Ligi Kuu Bara na ile ya kimataifa huku hadi sasa ikinasa saini ya nyota kadhaa wakiwemo, Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza na Nassoro Kapama aliyetokea Kagera Sugar.

Mbali na Usajili huo taarifa za kuaminika zinadai kuwa nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni mshambuliaji raia wa Uganda, Cesar Manzoki aliyetokea (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko ya Ghana.

KUPITIA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, SLOTI YA STICKY 777 INAWEZA KUKUPA FAIDA KUBWA! PAMOJA NA RAIS WA YANGA INJINIA HERSI KUKATAA MAYELE KUSEPA…WAARABU BADO WAVIZIA NAMNA YA KUSEPA NAYE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply