UBORA wa benchi la ufundi la Klabu ya Yanga chini ya kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedrick Kaze ni moja ya sababu inayomfanya Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mshindo Msola kufanya nao kazi.
Msola amemaliza muda wake wa uongozi wa kiti hicho jana Julai 9 akitoa neno la shukrani kwa wanayanga wote waliokuwa bega kwa bega.
Msola amesema ataendelea kufanya kazi na Kaze pamoja na Nabi japokuwa hayupo ndani ya Yanga kama kiongozi.
“Nitafanya nao kazi Nabi na Kaze nikiwa nje ya Yanga, amesema Msola”.
Msola amesema atafanya hivyo kutokana na taaluma yake ya ukocha aliyonayo.
Mafanikio ya Yanga msimu huu yamechangiwa na ubora wa benchi hilo la ufundi lililotengeneza ubora wa wachezaji wa timu hiyo.
Ubora huo umeifanya Yanga kutwaa tuzo nyingi juzi huku nyota wao Yanick Bangala aking’ara baada ya kuibuka na tuzo ya mchezaji na kiungo bora wa msimu.