Habari za michezo

KISA RONALDO…MESSI AWAPIGWA MKWARA PSG…AWAAMBIA WAKIMSAJILI TU..NA YEYE ANASEPA SIKU HIYO HIYO…

admin July 10, 2022 4:54 pm


Ripoti zinaeleza kuwa, staa wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi, ametishia kuondoka kikosini hapo endapo klabu hiyo itamsajili Cristiano Ronaldo.

Kwa sasa Ronaldo anatajwa kuondoka Manchester United, huku PSG ikiwa ni kati ya timu ambazo zinatajwa kumuwania sambamba na Chelsea na Bayern Munich.

Imeelezwa kuwa, hakuna uhakika kama PSG itatishika na suala hilo la Messi kwani timu hiyo inataka kujipanga kuona inafanya kweli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini imeelezwa kuwa, uwepo wa Kylian Mbappe kwenye projekti mpya kunaweza kumvuta Ronaldo ndani ya kikosi hicho, Messi na Ronaldo wamekuwa washindani wakubwa kwenye soka ambapo wanatajwa kuwa ni wachezaji wenye rekodi za kutisha.

Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye Ballon D’or nyingi akiwa nazo tano, huku Messi akiongoza akibeba saba.

KISA SOPU NA AKPAN….COASTAL UNION WAZIKAMUA SIMBA NA AZAM ZAIDI YA MILIONI MIA MBILI… BAADA YA KUMTAMBULISHA MBURUNDI WA NEWCASTEL JANA…MASHINE NYINGINE HII HAPA ITATUA YANGA…BANDO MUHIMU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply