Habari za michezo

ISHU YA KUMSHAMBULIA RAIS KARIA YAMSOTESHA MANARA TFF…AWEKWA MTU KATI….MASHAHIDI WAFUNGUKA A-Z….

admin July 12, 2022 2:34 am


Mashahidi waanza kutoa ushahidi wa tukio la Msemaji wa Yanga Haji Manara dhidi ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

Ilitokea sintofahamu Juni 29 wakati wa fainali ya kombe la FA iliyoikutanisha Yanga na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ilionekana wawili hao wakizozana katika video iliyosambaa mitandaoni huku watu wakimtuliza Manara.

Julai 3 Sekretarieti ya TFF ilifungua shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

Habari ambazo zina uhakika zinadai kuwa tayari kesi huyo imeishaanza kuunguruma na mashahidi wameanza kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo.

Mmoja wa mashahidi alipotafutwa kudokeza undani wa sakata hilo alikaririwa akisema juu ya kushangazwa na namna mzozo huo jinsi ulivyoibuka.

Licha ya Manara kukutana na Karia na kuomba msamaha na kuomba hadharani akikiri kukosea kamati imeendelea na kesi hiyo.

RASMI….FIFA WAMTAJIRISHA MSUVA CHAP CHAP….WAARABU WAAMRIWA WAMLIPE BILIONI 1.6…ISHU NZIMA IKO HIVI…. KUELEKEA MSIMU UJAO…MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO…WAANZA KUTEMBEA NA ‘BITI’ LA SIMBA NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply