Habari za michezo
RASMI….FIFA WAMTAJIRISHA MSUVA CHAP CHAP….WAARABU WAAMRIWA WAMLIPE BILIONI 1.6…ISHU NZIMA IKO HIVI….
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza Club ya soka ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa Mchezaji Mtanzania Simon Msuva zaidi ya dola za kimarekani laki saba (zaidi ya Tsh bilioni 1.6) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Club hiyo.
Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake December mwaka 202 kutokana na kuidai Club hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).
Aidha, imeelezwa kuwa hukumu ya FIFA imeamuru Mchezaji huyu alipwe na riba pia.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.