Home Habari za michezo KOCHA MPYA SIMBA AANZA NA MKWARA KWA YANGA…ATAMBIA REKODI YA KUCHEZA MECHI...

KOCHA MPYA SIMBA AANZA NA MKWARA KWA YANGA…ATAMBIA REKODI YA KUCHEZA MECHI ZA DABI MBELE YA UMATI…


Kocha Mkuu wa Simba SC Zoram Maki amesema yupo tayari kwa mchezo wa Dabi dhidi ya Young Africans utakaopigwa Agosti 13, Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.

Miamba hiyo ya Kariakoo itapapatuana kwenye mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii, ambao pia utatumika kama kiashirio cha kufungua msimu wa 2022/23.

Kocha Zoran amejinasibu kuwa tayari kwa mchezo huo alipojibu swali la Mwandishi wa Habari katika Mkutano Maalum wa Kumtambulisha uliofanywa leo Jumanne (Julai 12), Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Kocha huyo kutoka nchini Serbia amesema amekua na uzoefu na michezo ya Dabi, na kila alipofundisha soka katika Bara la Afrika amepata Joto la michezo hiyo.

Amesema aliwahi kukutana na Joto hilo nchini Angola, Alegria, Morocco na Sudan, hivyo kwake ni jambo la kawaida na wala haofii mchezo dhidi ya Simba SC.

“Nimefundisha Soka Barani Afrika, kwa bahati nzuri kila nilipokwenda nimekutana na changamoto ya Dabi, nilipokua Angola nafundisha klabu Primeiro de Agosto niliwahi kucheza dhidi ya Petro Atlético [Mashabiki 50,000], Nikiwa Morocco na klabu ya Wydad Casablanca nilicheza dhidi ya Raja Casablanca [Mashabiki 70,000], Sudan nilipokua na Al Hilal nilicheza dhidi ya Al Mereikh [Mashabiki 50,000] na Algeria nilipokua na CR Belouizdad nilicheza dhidi ya USM Algiers [Mashabiki 40,000],”  

“Hata hapa Tanzania kuna Dabi nzuri sana kati ya Simba na Young Africans, hivyo popote utakapofanya kazi unatakiwa kujiandaa na Dabi, kwa hiyo unatakia kuwa na muda mzuri wa maandalizi.” Amesema Kocha Zoran

Kipimo cha kwanza kwa Kocha Zoran akiwa na Simba SC atacheza dhidi ya Young Africa katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii Agosti 13, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  MORRISON, MANULA NA ONYANGO OUT SIMBA....LWANGA NDANI SAFARI YA SIMBA ZANZIBAR...