Home Habari za michezo SIKU KADHAA TOKA ASAJILIWE NA MASHABIKI KUANZA KUMKATAA..KIGOGO SIMBA AIBUKA NA HILI...

SIKU KADHAA TOKA ASAJILIWE NA MASHABIKI KUANZA KUMKATAA..KIGOGO SIMBA AIBUKA NA HILI KUHUSU KYOMBO…


Wakati mashabiki wa Simba wakionyesha kutoukubali usajili wa mshambuliaji Habib Kyombo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mulamu Nghambi amewatuliza na kuwaambia wasubiri tu, kwani walichokifanya sio kama wamebahatisha.

Kyombo alitambulishwa juzi, akitokea Mbeya Kwanza baada ya awali kusaini pia Singida Big Stars, huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakiwaka kupitia mitandao ya kijamii, lakini Mulamu alifichua dili la mchezaji huo na sintofahamu yake, huku akiwatuliza mashabiki hao.

Akizungumza Mulamu amesema kuwa; “Wasichokijua watu wengi Kyombo ni mchezaji aliyewahi kucheza Simba B, hivyo amerejea nyumbani, ndio maana yeye akaomba avunje mkataba wake na SBS aliposaini hapo awali,” alisema Mulamu na kuongeza;

“Jambo lingine hakusaini sehemu mbili ila baada ya kuona viongozi wa Simba wamemfuata ndipo alipoamua kwenda kuuvunja mkataba wake mwenyewe na Singida Big Stars alikosaini miaka miwili ndio maana suala lake limeisha kwa amani.”

Mbali na hilo, aliwatoa mashabiki wao hofu na kusisitiza kuna silaha watazishusha ambazo zitakosha mioyo yao hivyo wasihangaike wala kupata presha na kile kinachoendelea kufanywa na wapinzani wao kwani hawasajili kwa mihemko.

“Simba ni levo nyingine na tulishaachana na tabia za kushindania wachezaji, tuna watu wanaofanya skauti za maana kulingana na mahitaji ya timu yetu, mashabiki zetu watulie na waunge mkono juhudi ambazo zinazofanywa na viongozi wao,” alisema Mulamu.

Kyombo aliwahi kung’ara na Mbao, Singida United zilizoshuka daraja kabla ya kwenda Afrika Kusini na aliporejea alijiunga na Mbeya Kwanza iliyoshuka pia msimu huu na katika mechi 12 alizoichezea alifunga mabao sita, ikiwa na wakati kila mechi mbili alifunga bao moja.

SOMA NA HII  YANGA LETENI YEYOTE TUNAPIGA TU...MORRISON, SAKHO WAMTISHA BOSI ORLANDO...IBENGE NA MAYELE....