Habari za michezo

DK KIGWANGALA AFUNGUKA BIFU LAKE NA MO DEWJI…ADAI AMEPIGIWA SIMU NA KUPEWA ‘UPDATES’ KUHUSU MENGI YA SIMBA..

admin July 15, 2022 6:06 pm


Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mwanachama wa Klabu ya Simba amesema hana ugomvi na mtu isipokua anachotaka kuona kikifanyika ni uendeshaji ulio wazi ndani ya klabu hiyo na kwamba anachofanya sasa ni kuitumia haki yake ya kikatiba ibara ya 100 na ibara ya 18.

Kigwangalla ameandika; “Sina ugomvi na Mtu, ningekuwa na ugomvi mfano na Mooo ningemshambulia yeye ‘binafsi’ akini sijafanya hivyo, hata pale aliponidhalilisha sikumlipizia, ninachotaka ni mifumo ya uendeshaji iwe wazi bila janjajanja, natumia haki yangu ya kikatiba ibara ya 100 na ibara ya 18.”

Vilevile Kigwangalla amesema amepigiwa simu na Mwenyekiti wa Simba SC kupewa updates juu ya mambo mengi ya klabu hiyo na nina mnukuu alichoandika.

“Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC amenipigia kunipa updates juu ya mambo mengi ya klabu yetu, pamoja na kwamba kuna baadhi ya mambo sikuridhishwa na yalivyowekwa hususan yale ya kiuwekezaji, ya usajili yako vizuri sana tu, walau ameonesha ujasiri, uwazi na weledi wake,” amesema Kigwangalla.

PAMOJA NA KUCHUKUA MAKOMBE YOTE ….NABI KAONA HAITOSHI….ATAKA NA  MAKOCHA WA SIMBA … BENCHI LAMFANYA MPOLE KUTEMBEA NA MKATABA WA SIMBA KWENYE BEGI….AFUNGUKA HAYA KUHUSU HATMA YAKE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply