Habari za michezo

SINGIDA BIG STARS WAANZA KUONYESHA MAKUCHA YAO YA USAJILI…’WAMKWAPUA’ KIPA AZAM MCHANA KWEUPEEE…

admin July 15, 2022 4:04 pm


Aliyekuwa kipa wa Azam FC, Benedict Haule ‘Beko’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Singida Big Stars katika msimu ujao.

Beko amemaliza mkataba na Azam ndipo Uongozi wa Singida ukaona umuongeze katika kuimarisha eneo la kipa.

Usajili wa Beko kwenye kikosi hicho unaenda kuimarisha eneo la kipa kwani tayari alishasajiliwa Metacha Mnata kutoka Polisi Tanzania.

Akizungumzia usajili wake, Beko amesema ni jambo zuri kujiunga na timu huku akiweka wazi imani yake ni kufanya vizuri.

Beko amesema ana imani kubwa atakuwa sehemu ya wachezaji ambao wataisaidia timu hiyo kuwa miongoni mwa timu tishio.

“Mpaka nasajiliwa Uongozi umeona umuhimu wangu kuwa hapa, upande wangu sitowaangusha nitahakikisha naipambania timu,”amesema Beko.

Kipa huyo aliwahi kucheza katika timu za Mbao, Prisons na Azam FC kwa nyakati tofauti.

KISA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA….BOSI SportsPesa ATAMBA KUIPA YANGA UDHAMINI WA KIHISTORIA…DAU LAKE SIO POA… BAADA YA KUTUA MISRI SALAMA…KOCHA MPYA SIMBA ATAMBA KUPIKA ‘TIMU LA MAUAJI’ KWA WIKI TATU TU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply