Habari za michezo

KISA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA….BOSI SportsPesa ATAMBA KUIPA YANGA UDHAMINI WA KIHISTORIA…DAU LAKE SIO POA…

admin July 15, 2022 4:00 pm


Baada ya miaka mitano ya Udhamini wa Sportpesa, klabu ya Yanga inatarajiwa kusaini mkataba mwingine wa miaka mitano kuendelea na udhamini wa kampuni hiyo

Mapema jana klabu ya Simba ambayo pia ilikuwa ikidhaminiwa na Sportpesa, ilitangaza kusaini mkataba wa miaka mitano na M-Bet kuwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo.

Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Abbas Tarimba, amesema Mkataba ambao watasaini na Yanga utaweka rekodi kwani hakuna klabu yoyote hapa Tanzania iliyowahi kupata mkataba wa aina hiyo.

“Ni kweli mkataba tuliosaini awali umemalizika, hivi karibuni tutaingia mkataba mwingine mkubwa zaidi na wa kihistoria na klabu ya Yanga SC, ambao haujawahi kuingiwa na klabu yoyote,” alisema Tarimba

Katika mkataba uliopita, Yanga ilikuwa ikipokea takribani Tsh Bilioni 1 kila mwaka kutoka SportPesa.

Ni wazi katika mkataba huo mpya dau litaongezeka mara dufu.

BAADA YA WAARABU KUAMRIWA KUMLIPA FIDIA YA BIL1.6 ..MSUVA AWAPA SHARTI HILI GUMU…WAKIZINGUA FIFA INAWACHORA… SINGIDA BIG STARS WAANZA KUONYESHA MAKUCHA YAO YA USAJILI…’WAMKWAPUA’ KIPA AZAM MCHANA KWEUPEEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply