Geita Gold FC

PAMOJA NA KUFANYA KAZI NZURI MSIMU HUU…GEITA GOLD WAMTEGA ‘KININJA’ MINZIRO…AAMBIWA NI JUU YAKE KUJIMALIZA…

admin July 16, 2022 9:55 am


Hatma ya Kocha wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ iko mikononi mwake endapo ataona mkataba mpya unamfaa kuendelea kuinoa timu hiyo kwa msimu ujao.

Minziro baada ya msimu kumalizika kwa mkataba wake ulifika kikomo na sasa viongozi wako katika mipango ya kumuongezea ili aendelee kuliongoza jahazi la timu hiyo.

Akizungumza Mwenyekiti wa timu hiyo, Costantine Molandi alisema jana kuwa viongozi walikutana kwa mara nyingine kupanga mipango ya maandalizi ya msimu.

“Leo (jana) tutakuwa na kikao kingine na ndicho kitakuwa na maazimio ya timu iweke wapi camp (kambi) kwa ajili ya msimu ujao sambamba na masula ya usajili,” alisema Molandi.

Aidha Molandi alisema, ubora aliouonyesha Minziro ndani ya kikosi chao ulisababisha timu kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa imewafanya waendelee kuhitaji huduma yake.

“Tunachokifanya sisi ni kuongea nae na kumuonyesha ofa ya mkataba wetu, sasa akiamua kubaki ni yeye endapo ataona maslahi yanamruhusu, ila sisi tunatamani kuendelea naye,” alisema Molandi.

Minziro alipoulizwa juu ya hatima yake ndani ya kikosi hicho amesema:

“Bado hawajaniita mpaka sasa, tukielewana nitaendelea kuinoa timu.”

BAADA YA KUONA MASTAA WAPYA WA YANGA…CHAMA KATIKISA KICHWA WEEH….KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA… AUSSEMS AZIVURUGA KLABU ZA KENYA NA RWANDA….ADAIWA KUSAINI MKATABA BILA KUAGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply