Home Habari za michezo USAJILI NDANI YA YANGA….NABI ‘AVIMBA’ NA UJIO WA AZIZ KI….ADAI UTAMTIA PRESHA...

USAJILI NDANI YA YANGA….NABI ‘AVIMBA’ NA UJIO WA AZIZ KI….ADAI UTAMTIA PRESHA YA KUCHAGUA VIZURI…


Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amechekelea aliposikia rasmi mshambuliaji wake Stephane Aziz KI, ameshatua nchini na kutambulishwa lakini akafichua na jeshi alilonalo kuna kazi nzito msimu ujao.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Tunisia alipokwenda kwa mapumziko mafupi, Nabi alisema amekuwa na amani ya moyo baada ya kumuona Azizi KI akitambulishwa na sasa rasmi atakuwa naye kwa msimu ujao.

Nabi alisema Azizi KI ni mshambuliaji bora ambaye anakwenda kukamilisha ubora mkubwa ambao watakuwa nao kwa msimu ujao katika safu yao ya ushambuliaji.

“Niliwaambia kwamba atafika, nilihakikishiwa na Ghalib (Said) kabla ya kuondoka hapo Tanzania, mchezaji mwingine bora ameongezeka katika kikosi chetu,” alisema Nabi na kuongeza;

“Naamini ujio wa Azizi KI utatupa nguvu nyingine kubwa sana kuekekea msimu ujao ambao nauona utakuwa mgumu zaidi, kila timu inajipanga sawasawa, tutakuwa na safu bora ya ushambuliaji kwa ujio wa mchezaji huyu.”

Aidha Nabi alisema akiangalia usajili wao mpya na mastaa waliosalia kutakuwa na ushindani mkubwa wa nafasi kazi ambayo itaongeza presha kubwa hata kwao makocha.

Alisema amekuwa akijaribu kupanga timu hiyo kwenye makaratasi lakini amebaini sio kazi rahisi kwa kuwa wana timu bora zaidi kuekekea msimu ujao.

“Niko hapa nyumbani kuna wakati najaribu kutengeneza mipanmgo yangu kulingana na wachezaji tulionao lakini nikwambie tuna timu kubwa kuna presha kubwa pia kupanga hii timu,” alisema Nabi na kuongeza;

“Nafahamu sio kila wakati unaweza kuwa nao wote wakiwa kwenye ubora lakini pia kuna wakati watakuwepo wote na mbaya zaidi wakawa wote wanataka kucheza lazima uwe na saikolojia nzuri kwa kuzungumza na mchezaji anayebai nje, tuna timu bora sana.”

Yanga inatarajia kuanza kambi ikiwa jiji Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya kabla ya kukipuiga Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 13, ikiwa ni wiki moja tangu ifanye Wiki ya Wananchi.

SOMA NA HII  ASUKILE AIPIGA MKWARA KAMA WOTE SIMBA SC...AKUMBUSHIA KIPIGO CHA MSIMU ULIOPITA...