Habari za michezo

BAADA YA UJIO WA MASTAA KIBAO KITOKA NNJE..KIBU DENIS AIBUKA NA HILI KUHUSU NAFASI YAKE KIKOSI CHA KWANZA…

admin July 19, 2022 4:56 pm


Hadi sasa Simba imetambulisha wachezaji watano wapya lakini staa wake wa msimu uliopita, Kibu Denis hahofii kupoteza namba yake kwani anaamini msimu ujao atakuwa bora zaidi.

Ujio wa viungo washambuliaji, Mzambia, Moses Phiri, Mghana Augustine Okrah, Habibu Kyombo na Nassoro Kapama ambaye ni kiraka umeiweka rehani nafasi ya Kibu anayecheza nao nafasi moja sambamba na mastaa wengine Msenegal Pape Sakho na Mmalawi Peter Banda lakini mwenyewe haogopi.

Kibu aliyemaliza msimu uliopita akiwa kinara wa mabao ndani ya Simba akiibuka mfungaji bora wa timu hiyo kwa mabao yake nane na asisti nne ameweka wazi bado anaiona nafasi yake ndani ya Simba msimu ujao.

“Wote ni wachezaji wazuri lakini hawanifanyi mimi kukusa nafasi. Tupo hapa kupambania timu kwa pamoja kuhakikisha inafikia malengo hivyo nawakaribisha Simba,” alisema Kibu aliye kwenye kambi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ na kuongeza;

“Nashukuru sina majeruhi na naendelea na mazoezi. Nitazidi kufanya vizuri kila nikipewa nafasi na kumfanya kocha aweze kunipa namba mara kwa mara.”

Kibu alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Mbeya City aliyojiunga nayo kutoka Geita Gold ikiwa Daraja la Kwanza kwa kipindi hicho na kabla ya hapo aliwahi kuichezea Kumuyange FC ya Ngara ambayo baadae iliuzwa Dodoma na sasa inaitwa Fountain Gate.

ACHANA NA STORI ZA VIJIWENI..UKWELI KUHUSU DILI LA OUATTARA KUTUA SIMBA UKO HIVI…AL HILAL WATOA TAMKO… BAADA YA KIMYA KIREFU….HATIMAYE JINA LA NCHIMBI KUTAJWA TENA LIGI KUU AKIWA NA TIMU HII MPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply