Habari za michezo

RASMI…TFF WAMFUNGA MDOMO MANARA KWA MIAKA MIWILI….MANENO YA HOVYO KWA KARIA YAMPONZA MIL 20…

admin July 21, 2022 11:15 am


Kamati ya Maadili ya TFF imemhukumu Ndugu Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kipindi cha miaka miwili (2) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 20 [Tsh 20,000,000]. Adhabu hiyo inaanza leo Alhamisi, Julai 21, 2022.

Manara alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kuwakashifu viongozi wa TFF, kuwatolea maneno ya hovyo na kukiuka kanuni za maadili za Shirikisho la Soka Tanzania.

Katika video iliyosambaa siku ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, kati ya Yanga na Coastal Union katika Dimba la Sheikh Amri Abid jijini Arusha, Manara alionekana akirushiana maneno na Rais wa TFF, Wallace Karia hivyo kuitwa mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma ambazo zimemtia kitanzini hii leo.

Ikumbukwe kuwa, si mara ya kwanza kwa Manara kufungiwa, mwaka 2017 akiwa Ofisa Habari wa Simba SC, Manara amlifungiwa kutojihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi 12 na faini ya shilingi milioni 9, vyote kwa pamoja kwa makosa kama hayo.

SINGIDA BIG STARS NAO WANAJAMBO LAO AISEE…HANS PLUIJM APEWA MKATABA …LULE WA MBEYA CITY AKUBALI USAIDIZI… KUELEKEA TUZO ZA CAF LEO…PAPE SAKHO HUYU HAPA….MSENEGAL ANAYEIWAKILISHA TANZANIA NA SIMBA KIMATAIFA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply