Habar za Usajili Simba

RASMI….SIMBA NA VIPERS WAMALIZANA SAKATA LA KUMSAJILI MANZOKI…KITUO KINACHOFUATA NI HIKI HAPA…

admin July 22, 2022 9:25 am


Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Ceazer Lobi Manzoki anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba SC kambini mjini Ismailia-Misri, kufuatia suala lake la uhamisho kutoka kwa Mabingwa wa Uganda Vipers SC kuwekwa sawa.

Usajili wa Mshambuliaji huyo mzaliwa wa DR Congo uliingia dosari kufuatia viongozi wa Vipres SC kumzuia kwa kigezo cha mkataba wake uliokua umesalia muda wa miezi miwili.

Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa, Viongozi wa Klabu hiyo ya Msimbazi wamemalizana na Vipers SC kwa kununua sehemu ya mkataba wa Mshambuliaji huyo, na sasa yupo huru kuelekea Misri kwa ajili ya kambi.

“Baada ya kuona hali hiyo, tulimteua mjumbe mmoja akaenda Uganda kulipa kiasi cha pesa ambacho Vipers SC walikihitaji kwa ajili ya kuvunja mkataba wa Manzoki, tumefanikisha hilo bila tatizo lolote,”

“Kwa sasa Manzoki yupo huru kujiunga na Simba SC, moja kwa moja ataelekea Misri kwa ajili ya kuanza mazoezi na wenzake ambao tayari wana juma moja tangu walipoanza kambi chini ya Kocha wetu Zoran Maki.”

“Manzoki ni miongoni mwa wachezaji watatu wapya ambao bado hawajatambulishwa akiwepo Nelson Okwa na Mohamed Ouattara, ambao muda wowote kuanzia sasa watatambulishwa kwa mashabiki wetu.” Kimeeleza chanzo cha habari kutoka Simba SC.

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam Agosti 05, kwa ajili ya sherehe za Simba Day, ambapo kitacheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki siku hiyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

BAADA YA MANARA KUHUKUMIWA JANA….YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…WATOA TAMKO ZITO….WAAPA KUCHUKUA HATUA… BAADA YA YANGA KUJAA MASTAA WA KAZI KAZI…YACOUBA SOGNE ACHONGEWA MCHONGO WA KUTUA GEITA GOLD…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply