KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Ghana, Bernard Morrison, ‘amewatishia bastola ya maneno’ mabeki atakaokutana nao msimu ujao akiwemo beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe.
Morrison alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza, Januari 15, 2020 kabla ya mkataba wake kuleta mgogoro na baadaye Agosti 8, 2020 akatimkia Simba ambako amehama tena na kurudi Jangwani baada ya makataba wake kumalizika.
Morrison alisema kuwa, kufuatia uzito wa mazoezi anayoyafanya kwa sasa kwao nchini Ghana, ana uhakika beki yoyote atakayepangwa naye mara baada ya kurudi Bongo atamsumbua vibaya tofauti na walivyomzoea awali.
Aliongeza kuwa, anajinoa vikali kuhakikisha kuwa msimu ujao anakuwa zaidi ya alivyokuwa misimu iliyopita kwani anaamini katika mazoezi makali na sio vitu vingine.
“Ninafanya mazoezi huku Ghana ya kutisha sana, kiasi kwamba kama kocha atakuja kunipa nafasi ya kucheza mechi zijazo, basi mabeki nitakaokabana nao wajipange kutema damu.