Azam FC

KAULI HII YA SOPU KWA AZAM FC NI KAMA MASTAA ULAYA WANAVYOFANYAGA WAKISAJILIWA TIMU MPYA…

admin July 25, 2022 2:44 am


Baada ya kusajiliwa Azam, straika, Abdul Sopu ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa msimu ujao.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha kubwa kutokana na kiwango alichoonyesha akiwa na timu ya Coastal Union ya Tanga.

Sopu alikuwa mchezaji nyota kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho, huku akifanikiwa kufunga goli tatu kwenye mchezo huo.

Akizungumzia hilo, Sopu amesema kuwa “Ni furaha kubwa kwake kujiunga na klabu hiyo na haukuwa uamuzi mgumu kwa upande wake.

“Kujiunga na Azam haikuwa ngumu kwangu kwani ni timu yangu ya nyumbani, ni furaha kubwa kwangu kuwa hapa nawaomba mashabiki watusapoti kwani tumepanga kuwapa furaha kwa msimu ujao.”

Mara nyingi mastaa wa Ulaya wanaposajiliwa na timu nyinginezo, hata kama itafahamika kuwa walikuwa ni wapenzi wa klabu fulani, utasikia wakisema hizo timu walizosajiliwa ni timu zaopendwa toka walipokuwa wadogo, kauli ambayo mara nyingi huonekana ni ya ‘kimchongo mchongo’ hivi.

MORRISON NA AZIZ KI WAUNGANA KUWA WAKARIBISHA WAGENI YANGA…MOLOKO ‘APATWA UBARIDI’ NA USAJILI WA MASTAA WAPYA… USAJILI AZAM, SIMBA NA YANGA NI VITA YA MATAJIRI WATATU BONGO…MORRISON ATENGUA NAMBA YA MTU HUKO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply