Habari za michezo

TARIMBA AITAJA SIMBA KWA HILI WAKATI SportsPesa WAKISAINI MKATABA NA YANGA…

admin July 27, 2022 1:29 pm


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas Tarimba amesema Kampuni ya Sportpesa ndiyo Kampuni pekee ya michezo ya kubashiri iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia vilabu vya Simba SC na Young Africans kujiimarisha kiuchumi kupitia udhamini wao lakini pia kupitia mashindano ya Sportpesa tangu mwaka 2017.

Tarimba amesema hayo wakati wa hafla ya kusaini mkataba mpya na Klabu ya Young Africans leo Jumatano (Julai 27) jijini Dar es salaam.

Kuhusu Mkataba mpya, Kiongozi huyo wa SportPesa amesema, Klabu ya Young Africans itanufaika na Mkataba huu kwenye vipengele kadhaa ikiwemo endapo Klabu hiyo itashinda taji la Ligi Kuu ya NBC basi itafanikiwa kunyakua kitita cha Shilingi milioni 150.

Amesema Klabu hiyo pia itafanikiwa kunyakua kiasi cha shilingi milioni 75 endapo tu itafanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Kwa upande mwingine Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said ameipongeza Kampuni ya Sportpesa chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Abbas Tarimba kwa kufikia makubaliano hayo ya kihistoria kwa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.

Hersi ameahidi kusimamia maelekezo na makubaliano ya mkataba huo na kusisitiza kuwa Young Africans ipo tayari kufanya mambo makubwa zaidi na Kampuni ya SportPesa.

YANGA NA SportsPesa KIMEELEWEKA…WASAINI MKATABA MNONO KUZIDI WA SIMBA NA MBET… KWA MADILI HAYA YA KIBABE….YANGA NI WAKISHUA…SportPesa NA AZAM MEDIA WAIJAZA MABILIONI YA PESA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply