Baada ya kuwepo na maswali mengi kuhusu alipo kiungo wa Simba SC, Sadio Kanoute, msemaji wa klabu hiyo ameibuka na kutoa ufafanuzi kupitia ukurasa wake wa Instagram.
βYuko wapi Sadio Kanoute mbona hatumuoni Pre Season??! Kanoute alirejea kwao Mali kwa ajili ya kubadilisha Hati yake ya kusafiria (Passport) ambayo imekaribia kujaa.
Lakini kumekua na changamoto ya kupata Passport mpya kwa wakati na haraka kutokana na hali ya mambo nchini mwao. Leo amerejea Dar es Salaam na ameanza taratibu za kuja Misri kujiunga na wenzie.β