Habari za michezo

BAADA YA KUONA UWEZO MKUBWA WA LOMALISA…KIBWANA SHOMARI ATETEMEKA …AMATANGAZIA VITA VYA ‘KILUGURU’…

admin July 30, 2022 2:55 am


Beki wa Yanga, Kibwana Shomari ni kama ametangaza vita baada ya kusema hana wasiwasi na ujio wa beki Joyce Lomalisa kwenye kikosi hicho.

Kibwana mwenye uwezo wa kucheza beki wa kulia na kushoto, msimu uliopita alicheza zaidi kushoto na kuwaweka benchi Yassin Mustapha na David Bryson ambao baadaye walikuwa wanasumbuliwa na majeraha.

Ujio wa Lomalisa unatishia uwezekanao wa Kibwana kupata namba lakini ametamka kwamba kila mmoja atumie vizuri nafasi anayopewa.

“Ni kitu kizuri kuja kwake kwenye timu, mimi nikipata nafasi nitaonyesha nilichonacho ili kuisaidia timu kufanya vizuri,” alisema Kibwana na kuongeza;

“Kweli wameimarisha eneo hilo na lengo ni timu kupata mafanikio na hilo sio suala geni kwenye mpira kwani mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni kawaida.”

Kuhusu kucheza nafasi mbili tofauti alisema; “Kama mchezaji unatakiwa unapopewa nafasi tofauti na uliyozoea basi unatakiwa kumsikiliza kocha nini anakuambia na ufuate maelekezo, naamini nilifuata maelekezo ndio maana nikawa nacheza.”

‘MAVITUZ’ YA OKRAH YAMTIA WASIWASI BEKI KISIKI YANGA…AFUNGUKA WATAKAVYOTESWA NAYE KWENYE MECHI ZA LIGI… NDALA AANIKA ALIYOYAONA KAMBI YA AZAM NCHINI MISRI…ATOA ONYO KWA MASTAA WAPYA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply