Habari za michezo

MAYELE AENDELEA ALIPOISHIA …ATIA KAMBANI GOLI TATU MWENYEWE….AZIZ KI , MAKAMBO WANOGESHA ‘SHOW’….

admin July 30, 2022 2:44 am


Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana Ijumaa, Julai 29, 2022.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Yanga katika maandalizi ya kuuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC inayotarajiwa kuanza kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba mnamo Agosti 13, 2022.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Kalala Mayele ambaye amepiga hattirick (mabao matatu), Stephane Aziz KI amefunga bao moja na Heritier Ebenezer Makambo ambaye pia amefunga bao moja.

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2021/22 wameweka kambi yao katika maskani yako yaliyopo Avic Town Kigamboni Dar, huku mahasimu wao Simba wakijichimbia katika mji wa Ismailia nchini Misri.

OKWA ATUA SIMBA KIBABE SANA…KAGERE NA WENZAKE WARUDI DAR…BANGALA ATUA TZ KWA MKWARA…JEZI MPYA GUMZO …. ‘MAVITUZ’ YA OKRAH YAMTIA WASIWASI BEKI KISIKI YANGA…AFUNGUKA WATAKAVYOTESWA NAYE KWENYE MECHI ZA LIGI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply