Habari za michezo

‘KIZIZI’ CHA MAYELE CHAENDELEA KUFANYA KAZI BONGO….ATUPIA TENA YANGA IKIUA MTU GOLI TISA BILA…

admin July 31, 2022 12:45 pm


Yanga imecheza mchezo wa pili wa kujipima nguvu wakishusha kipigo kizito kwa Friends Ranger wakishinda kwa mabao 9-0.

Mchezo huo ambao umepigwa leo asubuhi mshambuliaji Fiston  Mayele ameendelea kutetema akipiga bao moja katika mchezo huo huku Lazarous Kambole naye akifungua akauti ya mabao.

Mabao mengine yamefungwa na kiungo Khalid Aucho na mshambuliaji kinda kutoka timu B Clement Francis wote wakifunga mara mbili kila mmoja.

Wengine waliocheka na nyavu katika ushindi huo ni pamoja na winga Denis Nkane, Jesus Moloko na Yacouba Sogne kila mmoja akifunga bao moja katika mchezo huo ambao Yanga walionekana kutawala.

Huo unakuwa ni ushindi wa pili wa Yanga ndani ya wiki moja tangu waanze kambi yao ya maandalizi ya msimu ambapo Julai 29 walicheza dhidi ya Transit Camp ambapo mabingwa wao walishinda kwa mabao 5-1.

WAKATI WATU WAKIHISI PENGINE NI MORRISON..SENZO AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUTEMANA NA YANGA…ADAI HAKUWA NA JINSI ZAIDI YA KUFANYA HIVYO… BANGALA ARUDI YANGA NA MZUKA KAMA WOTEE…AKUTANISHWA NA GSM WAKUBALIANA MAMBO HAYA MAPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply